Athari za joto kali kwa afya ya mtoto aliye tumboni


Viwango vya juu vya joto vinaweza kuathiri afya ya kijusi tumboni. Kulingana na utafiti wa hivi karibuni, mwanamke mjamzito anayefanya kazi katika eneo lenye joto kali anaweza kumdhuru mtoto anayembeba tumboni.

Miongoni mwa athari zinaweza kujitokeza ni pamoja na: ongezeko la mapigo ya moyo ya kijusi na kupungua kwa kasi ya usambaaji wa damu  katika kiunga mwana (umbilical cord).    

Watafiti wanasema  mikakati yenye ufanisi inahitajika ili kuwalinda wanawake wajawazito  wanaokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi  yanayosababisha kupanda kwa viwango vya joto. Hali hii inayakumba maeneo mbali mbali ya dunia. 

Utafiti uliochapishwa katika jarida la  masuala ya kiafya Lancet Planetary Health, unafichua kuwa kila ongezeko la nyuzijoto  la joto la kupindukia husababisha  ongezeko la 17% la shinikizo kwa  kijusi tumboni.

 Ingawa utafiti umefanyika kuhusu athari za joto kwa wanawake wajawazito wanaoishi  katika nchi zinazoendelea, inaaminiwa kuwa  utafiti huu ni wa kwanza kuchunguza athari za  joto la juu kwa wanawake wazawazito wanaoishi katika nchi zenye pato la chini. 

 Wanawake wajawazito wanaofanya kazi katika mashamba ya mpunga katika eneo la  West Kiang, Gambia,  hushinda mashambani chini ya jua lenye joto kali kwa saa nane.

 Joto ni takriban 45°. Wakati wa msimu wa mvua, kiwango cha juu cha unyevunyevu husababisha joto ambalo ni vigumu kuhimili.

 Wataalamu, kwa usaidizi wa vifaa vya kupima afya yam tot tumboni - ultrasound , walirekodi kiwango cha joto cha vijusi.

Vipimo vilifanywa baada ya wanawake  kuanza   kazi  na  baada ya kumaliza siku ya kazi.

Wataalamu pia walichunguza athari za joto kwa akinamama. Kwa mfano: maumivu ya kichwa, uchovu na kichefuchefu. 

Dkt. Ana Bonell, mchunguzi mkuu katika LSHTM, alisema kuwa kuhangaika kwa kihusi kulishuhudiwa katika 33%  ya visa  katika mashamba  walikofanyia uchunguzi.

Dkt. Ana Bonell, mchunguzi mkuu katika LSHTM, alisema kuwa kuhangaika kwa kihusi kulishuhudiwa katika 33%  ya visa  katika mashamba  walikofanyia uchunguzi.

 “Tulishituka sana kubaini kuwa vijusi viliathiriwa na joto la juu,” alisema.

“Kwa pande wa kijusi, tuliona mapigo ya moyo yakiongezeka kwa viwango vya juu kupita kiasi. Hali mbaya sana. 

Tulishuhudia athari katika mzunguko wa damu. Kwasababu mfuko wa uzazi pia uliathiriwa na joto. 

 Kulingana na Doctor Bonell,  mabadiliko ya tabia nchi ndio sababu.  

“Ni muhimu kuhakikisha kwamba wanawake wote kote duniani wana mimba salama. Inapaswa kutambuliwa kuwa tukiwa na mabadiliko ya tabia nchi, tunakuwa na viwango vya juu vya joto, hususan mawimbi ya joto. 

 Kama hakuna kitakachofanyika, wanawake wanaoshinda  katika viwango vya juu joto wanakabiliwa na hatari watoto wanaugua wakati wa kuzaliwa. Pia tunaweza kutarajia uzazi wa mapema au kuzaliwa kwa watoto njiti.

 “Tuna matumaini kuwa utafiti huu utawanusuru wanawake wengi  na watoto wao. Lakini pia, mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia.  

Dkt. Bonell alisema kuwa utafiti zaidi unahitajika kuchunguza kwa athari za usambaaji wa damu katika kijusi.

 Ni muhimu kutambua athari za sumu zinazotengenezwa na mama wakati wa joto kali katika ukuaji wa kijusi.

Chanzo: BBC Swaahil


Post a Comment

Previous Post Next Post