Fahamu nchi 5 bora za kulelea watoto

 Kwa watu wanaotaka kuhamia nchi za kigeni ima ni kwenda kufanya kazi au kupata makazi ya kudumu, viwango vya maisha vya nchi husika ni baadhi ya masuala muhimu wanayozingatia. Lakini wanapoamua kuandamana na watoto kuna mambo ya ziada wanayozingatia kando kuangalia kwa mfano wastani wa mapato au utulivu wa kiuchumi.

Wazazi hususan wanataka kujua mazingira watakayolelea watoto wao, ubora wa elimu, sera za likizo ya familia - hata ni nchi zipi zina viwanja vya michezo.

Haya ni baadhi ya masuala ya ambayo shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef linazingatia katika "tathimi yake" kuhusu ustawi wa mtoto.

Ni muhimu kutambua kwamba viwango vyao vinaangalia tu nchi tajiri zaidi duniani - na sio data yote inaweza kuwa ya manufaa sawa kwa familia za nje.

Lakini matokeo yao yanasaidia kuchora taswira ya kina ya mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kuhamia nchi ya kigeni ukiwa na watoto au unapanga kuanza familia katika nchi ya kigeni.

Tumetumia baadhi ya utafiti huu ili kujaribu kujibu swali kuu la kila familia inayotaka kuhama: ni wapi mahali pazuri pa kulea watoto?

JapanJapan ni mojawapo ya nchi salama zaidi kwa familia, na watoto mara kwa mara kwenda shuleni peke yao.

Katika uchanganuzi wa Unicef wa mwaka 2020 kuhusu ustawi wa watoto, Japan inashika nafasi ya kwanza katika suala la afya kwa ujumla, ambayo inaangazia vifo vya watoto na unene uliopitiliza.

Na katika ripoti ya hivi punde -mwaka wa 2022, ambayo iliangazia hasa mazingira ambayo watoto wanakulia, inashika nafasi ya pili katika "ulimwengu unaomzunguka mtoto" - kitengo kinachojumuisha vipengele kama vile nafasi ya mazingira ya kuishi mijini na usalama wa barabarani.

Japan pia ina kiwango cha chini zaidi cha unene wa kupindukia kwa watoto, vifo vya chini vya watoto na viwango vya chini sana vya uchafuzi wa hewa au maji yanayoathiri watoto.

Pia ni moja ya nchi salama kwa familia, na sio tu katika suala la ajali za barabarani.

Visa vya mauaji kwa nchini Japan kwa ujumla viko chini sana kati ya nchi zozote ambazo Unicef ​​iliangazia katika utafiti wake ukilinganisha na Marekani Canada na Australia.

Usalama huo unapatia wanafamilia utulivu wanaohitaji kufanya kazi huku watoto nao wakifuraihia uhuru wao, kulingana na Mami McCagg, mzaliwa wa Tokyo ambaye sasa anaishi London.

Estonia

Mojawapo ya vivutio vikubwa zaidi vya Estonia kwa familia ni mfumo wake wa elimu.

Estonia haipo kileleni mwa viwango vya jumla vya Unicef, lakini ina viwango vya juu zaidi katika vipengele kadhaa muhimu.

Watoto wanakabiliwa na uchafuzi mdogo wa hewa, mazingira tulivu isiyo na kelele ikilinganishwa nchi nyingine yoyote tajiri. Ina eneo la kijani kibichi zaidi mijini kuliko mataifa mengine mengi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Canada, Australia na Uingereza, na watoto wana uwezekano mkubwa wa wanafurahia mazingira wanayokulia kwani wanapata vifaa kama vile viwanja vya michezo.

Mojawapo ya vivutio vikubwa zaidi vya Estonia kwa familia ni mfumo wake wa elimu.

Watoto wanapata ujuzi bora wa hisabati, sayansi na kusoma na kuandika kuliko nchi yoyote nje ya Asia.

Ujuzi wa kidijitali unasisitizwa pia. "Tayari katika shule za chekechea, wanajifunza kupitia roboti, kompyuta na kadhalika, zote zinatumika kama sehemu ya kujifunzaji wa kucheza," alisema Anne-Mai Meesak, meneja wa mradi katika bodi ya elimu na vijana ya Estonia ambaye anatafiti mifumo ya elimu ya msingi nchini.

Likizo ya familia: Estonia ina sera mojawapo ya ukarimu zaidi ya nchi yoyote duniani, ikiwa na siku 100 za likizo ya uzazi pamoja na siku 30 za likizo ya uzazi ikifuatiwa na siku 475 za likizo yenye malipo kwa wazazi, kugawanywa - au kutumika. kwa muda - hadi mtoto awe na umri wa miaka mitatu.

Kwa hadi siku 60 kati ya hizo, wazazi wote wawili wanaweza kukaa nyumbani kwa wakati mmoja na wote wawili walipwe.

Kila mzazi pia hupokea siku 10 za kazi kwa mwaka za likizo yenye malipo kwa kila mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 14. (Likizo hii inapatikana kwa wakazi wa kudumu na wa muda wa Estonia.

Uhispani    Uhispania inashikilia nafasi ya juu kwa mazingira yanayowazunguka watoto na vile vile ustawi wa kiakili wa watoto

Uhispania iliorodheshwa juu zaidi katika orodha ya Unicef ​​ya mazingira yanayowazunguka watoto, huku kukiwa na viwango vya chini vya magonjwa ya watoto kutokana na uchafuzi wa hewa au maji.

Na licha ya kuwa na matoleo duni ya jumla katika masuala ya kijamii, elimu na huduma za afya, kulingana na Unicef, watoto nchini Uhispania wana ustawi wa hali ya juu: nchi hiyo inashika nafasi ya tatu kwa ustawi wa kiakili wa watoto na ya nne kwa ujuzi wa kimsingi wa masomo na kijamii.

Uhispania pia inajivunia kuwa na viwango vya chini vya visa vya vijana kujiua ukilinganisha na hali ilivyokatika nchi zingine kama Marekani, Canada, Australia au New Zealand.

Finland

 Finland, ambayo iko katika nafasi ya tano kwa jumla katika orodha ya hivi majuzi zaidi ya Unicef, ina alama za juu sana katika vitengo mbili kati ya tatu - Lakini ni nambari moja katika "ulimwengu wa mtoto" (ambayo inaangalia jinsi mazingira yanavyoathiri watoto moja kwa moja, kama vile ubora wa hewa) , na nambari ya pili katika masuala ya "ulimwengu unaomzunguka mtoto" (ambayo huangazia vipengele vya mazingira ambayo mtoto hutangamana nayo, kama vile shule, hatari za ajali za barabarani na mahali pa kucheza).

Ni mojawapo ya nchi zinazofanya vizuri zaidi duniani katika masuala ya ujuzi wa kusoma na kuandika na hesabu Kwa watoto, na wazazi wana uwezekano mkubwa wa kuzingatia sana uhusiano wao na walimu wa watoto wao shuleni.

Kiwango chake cha vifo vya watoto wenye umri wa miaka 5-14 ni mojawapo ya viwango vya chini zaidi duniani, chini ya nusu ya hiyo nchini Marekani.

Na nch hiyo pia i inatoa likizo ya ukarimu kwaa wazazi, ikiwa ni pamoja na wiki nane za likizo ya uzazi yenye malipo, miezi 14 zaidi ya likizo ya wazazi yenye malipo inayogawanywa kati ya wazazi, na likizo ya ziada ya malezi ambayo inaweza kutumika hadi mtoto atakapofikisha miaka mitatu.

Uholanzi

Uholanzi inatoa angalau wiki 16 za likizo ya uzazi iliyoidhinishwa, inayolipwa kikamilifu na hadi wiki sita za likizo ya uzazi yenye malipo.

Uholanzi inasifa ya juu katika orodha ya jumla ya Unicef ​​ya ustawi wa watoto ni Uholanzi, ambayo inafanya vizuri haswa katika suala la afya ya akili ya watoto (ndio nambari moja) na ujuzi (ambapo inashika nafasi ya tatu).

Vijana tisa kati ya 10 wenye umri wa miaka 15 wanasema wana kuridhika na maisha nchini humo, idadi ambayo ni kubwa zaidi ikilinganishwa nchi zote zilizofanyiwa uchunguzi na Unicef, na wanane kati ya 10 wanasema wanapata marafiki kwa urahisi.

Chanzo: https://www.bbc.com/swahili/articles/c727q1l2v55o






1 Comments

  1. Sera mbaya zaidi ya Elimu ambayo inaweza kuwachafua wote na mengine yakasahaulika, ni ile hali yao ya kuwafundisha watoto mambo ya ushoga na Ngono.

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post