Viongozi Wamekosea Kumruhusu Benchikha Kwenda Shule, Bora Barbara Arudi Simba- Mchambuzi

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Justine Kessy amesema kuwa kitendo cha Kocha wa Simba SC, Abdelhak Benchikha kuiacha timu yake wakati huu na kwenda nchini kwao kwa ajili ya kozi ya siku tano ni utoto na ujinga.

Kessy amesema hayo baada ya viongozi wa Simba kumruhusu Benchikha kwenda Algeria kuhudhuria kozi hiyo ikiwa ni saa chache baada ya kupokea kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons wiki iliyopita katika Dimba la Jamhuri Morogoro.

“Mimi ninadhani kuna haja ya kumrejesha Brabra Gonzalez akwenye u-CEO wa kwa sababu uongozi thabiti pale Simba haupo kwa sasa, mambo ambavyo yanakwenda hakuna utaratibu. Kiongozi yeyote makini lazima aonekane mnoko kwa watendaji wake.

“Kitendo cha kocha kuiacha timu ikiwa inatoka kubanguliwa na Tanzania Prisons ambayo imetoka kubanguliwa, sijaona mantiki yake. Kulikuwa na dirisha dogo angeondoka akawaachia maocha wasaidizi.

“Kozi ya siku tano anakwenda ili iweje? Kwa nini asisome online? Dunia imekuwa kiganjani tusidanganyane. Ninaona kocha ana risk tu kwa sababu hata matokeo dhidi ya Coastal Union wameyapata lakini floor ya Simba, kuna kitu kilikuwa kinakosekana kwenye benchi lao. Simba haiku mahala pazuri.

“Hivi viporo ni muhimu Simba akashinda ili atengeneze gape dogo dhidi ya Yanga, unaruhusu kocha kama yule aondoke wakati timu imeanza kukaa vizuri licha ya wachezaji kusemwa kuwa wamezeeka? Amewatumia walewale kutengeneza timu nzuri.

“Mimi ninaona ni utoto na ujinga kutokujali professional. Kwangu mimi huwezi kuiacha ligi ikiwa katika kipindi kama hiki Duniani ukaondoka. Sasa hivi bado miezi miwili ligi iishe unamuona Pep Guardiola, Mikel Arteta, au Jurgen Klopp, au Ten Hag aiache timu aende kwenye kozi?

“Pitso Mosimane anaweza kufanya ujinga kama huu? Al Ahly wanaweza kukuelewa au FAR Rabat kocha Nabi aondoke aende kwenye kozi? Bingwa wa shirikisho CAFCC msimu uliopita, Bingwa wa Super Cup umempiga Al Ahly, benchikha unakwenda kozi?

“Halafu unatoka kabisa kwenye vyombo vya habari viongozi wanatuambia kocha amekwenda kwenye kozi? This is unprofessional, bora mngetudanganya jambo jingine. Kozi ipi hiyo? Simba inataka kozi ya siku tano?

“Kocha amekwenda kusoma darasa la tano ili afanye mtihani wa Taifa wa darasa la Tano wakati huku kwetu hata mtihani wa darasa la saba umefutwa? Kozi ya siku tano unataka uje umsome nani?

“Gamondi au Dube ambaye amekuchakaza tangu yuko kule, au Aziz Ki ambaye anakufurumua mawe kila siku ama Maxi ambaye ulishindwa kumkaba ama Pacome ambaye anakuburuza uwanja mzima halafu kuna Fei Toto, Sospiter Bajana, James Akamainko, Jibril Silah.

“Ukiniambia leo Benchika amekwenda kufanya kozi kwa ajili ya Tanzania Prisons inatisha lakini kama ni kwa ajili ya robo fainali ya CAFCL labda kuna Petro Atletico, Al Ahly ama Mamelodi.

“Kwa kozi ya siku tatu atakuwa amechelewa. Siku tano za kozi, siku mbili safari kwenda na siku mbili safari kurudi, hapo atakosekana kama siku 10, ambapo ni mechi mbili za ligi hatokuwepo, hii mbaya sana. Simba wanatakiwa wafanye kitu la sivyo msimu ujao mambo yatakuwa magumu zaidi,” amesema Jusine Kessy.



Post a Comment

Previous Post Next Post