Madaktari kutoka Marekani kutoa huduma za kibigwa Wilaya ya Tanganyika

 Madaktari bingwa kutoka nchini Marekani wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda Mkoa wa Katavi tayari kwa kuanza kutoa huduma za upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika.


                                       Na Paul Mathias-Katavi

MADAKTARI  bingwa 18 kutoka nchini Marekani wamewasili katika Mkoa Mkoa wa Katavi tayari kwa kuanza kutoa huduma za Kibigwa katika Wilaya ya Tanganyika.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Shabani Juma [kushoto] akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Madaktari hao Profesa Eddie Chan muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege Mpanda.

Madaktari bingwa 18 kutoka nchini Marekani wamewasili katika Mkoa Mkoa wa Katavi tayari kwa kuanza kutoa huduma za Kibigwa katika Wilaya ya Tanganyika.

Madaktari hao wakiongozwa na Profesa Eddie Chan akizungumnza baada ya kufika katika Uwanja wa Ndege Mpanda amesema kuwa lengo la kufika katika Wilaya ya Tanganyika ni kutoa huduma kwa Wananchi kwa magojwa ya Kibigwa.

''Tumefika tunatalajia kutoa huduma za upasuaji tunaimani tutatoa huduma hii kwa watu wengi zaidi mimi na timu yangu’’-Chan

Ameelezakuwa wao wapo tayari kutoa huduma za kibigwa kwa wananchi na wanamatalajio watapata wateja wengi zaidi na wapo tayari kuwahudumia.

Amesema Madaktari hao wabobezi wamegawanyika Katika makundi Mbalimbali ya utalamu lengo likiwa ni kuwahudumia wananchi kulingana na mahitaji yao.

''Tunamadaktari bigwa wa upasuaji,watalamu wa usingizi,hawa wote tutakuwa nao ili kuhakikisha wenye changamoto ya Magojwa yanayohitaji upasuaji tunawapatia huduma’’-Chan

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Dk Alex Mrema amesema kuwa Madaktari bingwa watakuwa katika hospitali ya Wilaya ya Tanganyika kuanzia Tarehe 6/4/2024 hadi 13/4/2024.

Amewaomba wanananchi wenye tatizo la upasuaji kufika katika hospitali ya Wilaya ya Tanganyika kwaajili ya kupatiwa huduma hiyo kutoka kwa madaktari hao.

Shabani Juma Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema kuwa ujio wa madaktari hao ni fursa kwa wananchi wa Wilaya ya Tanganyika hususani wenye matatizo ya upasuaji.




Post a Comment

Previous Post Next Post